1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD.Mwito watolewa wa kuwepo ushirikiano wa karibu

27 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCp4

Waziri mkuu wa Irak Nuri al maliki ametoa mwito wa ushirikiano wa karibu katika serikali yake na kudai kwamba wimbi la ghasia nchini humo linaonyesha kuwa nchi hiyo imegawanyika kisiasa.

Wakuu wa madhehebu ya Sunni, Shia na Wakurdi wameonekana katika televisheni ya kitaifa wote wakitoa mwito sawa wa kudumishwa hali ya utulivu nchini Irak.

Viongozi hao pia wameapa kuwasaka na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wale waliohusika na shambulio la wiki iliyopita katika wilaya inayokaliwa na jamii ya Washia mjini Baghdad ambako zaidi ya watu 200 waliuwawa.

Msafara wa waziri mkuu Nuri al Maliki ulishambuliwa kwa mawe wakati alipozuru eneo hilo kuwahani walfiwa.

Mauaji hayo ndio makubwa zaidi kutokea kwa wakati mmoja tangu majeshi ya Marekani yalipoivamia Irak.