1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Mkahawa bungeni washambuliwa

12 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAT

Mlipuaji mmoja wa kujitolea mhanga ameshambulia mkahawa katika majengo ya bunge mjini Baghdad kwenye eneo la ulinzi mkali la Green Zone.Mlipuko huo ulisababisha vifo vya watu watatu na kukiuka sheria za usalama katika eneo hilo lililo na ulinzi mkali.

Bomu hilo lilisababisha takriban watu 20 kujeruhiwa na wabunge wawili kufariki huku majeshi ya usalama ya Iraq na Marekani yakiimarisha juhudi za kulinda usalama katika mji mkuu.

Marekani imelaani kitendo hicho kilichotokea saa chache baada ya daraja moja mjini Baghdad kulipuliwa na kuzama katika mto Tigris.

Waziri Mkuu Nuri al Maliki alilaani shambulio hilo na Spika wa Bunge kutangaza kuwa kikao maalum kitafanyika hapo kesho ili kulaani ugaidi.

Eneo la Green Zone ndiyo makao ya serikali ya Iraq vilevile balozi za nchi za kigeni lina ulinzi mkali nao wageni hulazimika kutumia vitambulisho vilivyo na picha vilevile kupekuliwa katika vituo kadhaa.