1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Mashambulio Iraq yazidi kushuhudiwa

27 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOA

Makamu wa rais wa Iraq Adel Abdul-Mahdi ambaye anatokea madhehebu ya washia pamoja na waziri wa Ujenzi Riad Ghraib walijeruhiwa katika shambulio ambalo linashukiwa kuwa jaribio lililotaka kuwauwa.

Takriban watu sita waliuwawa na wengine zaidi ya 30 walijeruhiwa kwenye shambulio hilo lililolenga mkutano uliyokuwa ukifanyika kwenye wizara ya ujenzi mjini Baghdad.

Wakati huo huo baraza la mawaziri la Iraq limepitisha mswaada muhimu wa sheria ya mafuta ambapo utajiri wa raslimali hiyo utaweza kugawanywa miongoni mwa makabila na madhehebu yote ya kidini nchini humo.

Sheria hiyo baadae itawasilishwa bungeni kupigiwa kura na endapo itapitishwa inaweza kufungua njia kwa ya kuingia kwa mabilioni ya dolla katika vitega uchumi vyake vya kigeni na kufufua uchumi wake uliosambaratika.