BAGHDAD:Maafa mapya wakati Ashura yaendelea | Habari za Ulimwengu | DW | 31.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Maafa mapya wakati Ashura yaendelea

Zaidi ya watu hamsini wameuawa katika siku nyingine ya ghasia zilizo na misingi ya kidini nchini Iraq.Katika shambulio moja baya zaidi,watu 23 walipoteza maisha yao na wengine 60 kujeruhiwa katika mji wa Mandali pale mlipuaji mmoja wa kujitolea muhanga aliposhambulia msikiti mmoja wa WaShia.Mlipuko huo ulitokea wakati mahujaji walipokusanyika kuadhimisha shughuli ya kidini ya Kishia ya Ashura.Ashura ni maadhimisho ya kifo cha Imam Hussein mjukuu wake Mtume Muhammed (rehma na amani zimfikie).

Yapata watu wengine kumi na mbili walipoteza maisha yao na 28 kujeruhiwa wakati bomu moja lilipolipuka kwenye jaa la taka wakati Washia walipofanya shughuli za kidini mjini Khahaqin ulio na Wakurdi wengi kulingana na polisi.

Saa chache baadaye makombora yalishambulia mitaa miwili ya Wasunni wengi na kusababisha vifo vya watu 9 na kujeruhi wengine 30 katika shambulio lililoelezwa kuwa la kulipiza kisasi kwa mujibu wa polisi.

Wakati huohuo mgombea mtarajiwa wa urais nchini Marekani Senator Barrack Obama senata wa jimbo la Illinois anatoa wito wa majeshi ya marekani kuondoka nchini Iraq ifikapo mwisho wa mwezi wa machi mwaka 2008.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com