BAGHDAD:Damu inazidi kumwagika Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 06.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Damu inazidi kumwagika Irak

Baghdad:

Mtu mmoja ameuwawa na wengine 6 wamejeruhiwa gari liliporipuliwa hii leo mjini Baghdad.Polisi inasema shambulio hilo katika mtaa wa kibiashara wa Baghdad lililengwa dhidi ya mkuu wa vikosi vya polisi mjini humo.Hata hivyo major Jenerali Ali Yasser amesalimika.Wakati huo huo waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amesema ameingiwa na wasi wasi kutokana na hali namna ilivyo nchini Irak.Amesema wafuasi wa kiongozi wa zamani wa Irak wanaweza kumtukuza Saddam Hussein kama mtu aliyekufa shahidi.Katika mahojiano na gazeti la Bild,waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amesema kwa mara nyengine tena nchi yake haitatuma wanajeshi nchini Irak.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com