1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad.Bomu laripuka na kuuwa watu kadhaa leo asubuhi.

30 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCxl

Nchini Iraq, bomu lililoripuliwa mapema leo asubuhi katika uwanja uliojazana watu mjini Baghdad, limeuwa kiasi cha watu 29 na kuwajeruhi wengine 50.

Mripuko huo umetokea katika wilaya ya mji wa Sadr ambako wafanyakazi walikuwa wamejikusanya kwa ajili ya kusubiri kazi za kibarua.

Kuna taarifa zinazopingana kama mripuko huo ulisababishwa na mtu aliyejitolea muhanga ama bomu lililokusudiwa kutegwa pembezoni mwa bara bara.

Wanamgambo wa kishia wa kundi la Mahdi wanalaumiwa kwa kusababisha maafa kadhaa katika mji huo.