1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Askari 30 wameuwawa katika shambulio la bomu la jutitoa muhanga

Takriban polisi 30 wameuwawa asubuhi leo walipokuwa wanafanya mazoezi wakati mshambuliaji wa kujitoa muhanga alipojilipua.

Mshambuliaji huyo aliyekuwa amepanda baiskeli alijilipua karibu na kambi ya kaskazini mwa mji mkuu wa Baghdad.

Wakati huo huo vikosi vya serikali ya Irak vimeanza rasmi majukumu yake katika mji wa Karbala baada ya majeshi ya Marekani kukabidhi majukumu hayo.

Kati ya majimbo 18 nchini Irak, Karbala ni jimbo la nane sasa kuwa chini ya usimamizi wa vikosi vya usalama vya Irak biöa ya usaidizi wa vikosi vya Marekani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com