1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Amri ya kutotoka nje baghdad yaondolewa

7 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvK

Amri ya kutoendesha magari katika barabara za mji wa Baghdad na maeneo mengine ya Iraq iliyowekwa kufuatia hofu kwamba huenda kukazuka machafuko kutokana na hukumu dhidi ya rais wa zamani wa Iraq itaondolewa leo.

Maafisa wa serikali wamesema tayari amri ya kuwazuia watu kutotembea katika baadhi ya maeneo nchini humo imeondolewa.

Amri hiyo ililengwa kuzuia ghasia baada ya mahakama kumkuhumu kifo bwana Saddam Hussein baada ya kumkuta na hatia ya uhalifu dhidi ya binadamu kutokana na kuhusika katika mauaji ya washia 148 mwaka 1982 katika kijiji cha Dujail.

Hata hivyo amri ya kuwazuia watu kutotoka nje wakati wa usiku mjini Baghdad bado itaendelea kuwepo.