1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Watu watatu wameuwawa kwenye shambulio la bomu

2 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCDE

Watu watatu wameuwawa leo na wengine kumi kujeruhiwa katika eneo la magharibi mwa mji mkuu Baghdad nchini Irak.

Bomu lililokuwa ndani ya motokaa iliyokuwa imeegeshwa nje ya gereji liliripuka katika eneo la Baiyaa linalokaliwa na Washia na Wasunni.

Duru za polisi zinasema motokaa tano na majengo yaliyo karibu yameharibiwa na mripuko huo.

Eneo hilo limekuwa kitovu cha operesheni za kuwasaka wapiganaji wa kisunni ambao wamekuwa wakiendeleza kampeni yao ya mashambulio ya mabomu katika juhdi za kuuvuruga mpango wa usalama wa jeshi la Marekani na Irak ambao umekuwa ukiendelea kwa majuma saba sasa.