1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Watu wasiopungua 122 wauwawa Irak

30 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCEA

Watu wasiopungua 122 wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa nchini Irak katika msururu wa mashambulio ya mabomu yaliyofanywa na watu wa kujitoa mhanga maisha mjini Baghdad.

Zaidi ya watu 60 wameuwawa kwenye soko moja mjini humo. Mabomu matatu yaliyokuwa ndani ya motokaa yaliripuka katika mji wa Khalis unaokaliwa na Washia kaskazini mwa mji mkuu Baghdad, na kuua watu 40. Mashambulio hayo yanafuatia mashambulio mengine mawili ya mabomu katika eneo la Washia la Tal Afar yaliyofanywa mnamo Jumanne iliyopita.

Watu 85 waliuwawa katika hujuma hizo zilizosababisha mashambulio ya kulipiza kisasi yaliyofanwa na Washia waliowapiga risasi na kuwaua Wasunni 70.

Idadi ya watu waliouwawa nchini Irak imekaribia 400 katika siku tatu zilizopita huku wapiganaji na makundi ya waasi wakikabiliana katika mapigano makali mjini Baghdad na vitongoji vyake.