BAGHDAD. Watu kumi wauwawa kwenye mlipuko wa bomu | Habari za Ulimwengu | DW | 15.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD. Watu kumi wauwawa kwenye mlipuko wa bomu

Watu kumi wameuwawa kufuatia mlipuko wa bomu katika mji mkuu wa Baghdad.

Bomu hilo limelipuka karibu na afisi za wizara ya mambo ya ndani, watu kadhaa wamejeruhiwa katika mlipuko huo.

Wakati huo huo kundi la watu waliotekwa nyara nchini Irak kutoka kwenye kituo cha utafiti wameachiliwa huru.

Vyombo vya habari nchini Irak vimemnukuu waziri mkuu Nuri al Maliki ametoa taarifa kwamba watu hao waliachiliwa huru mapema leo.

Utekaji nyara huo ulifanyika mchana na watu waliovalia mavazi rasmi ya polisi.

Maafisa wengi wa polisi walikamatwa baada ya mkasa huo kutokea hapo jana.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com