1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: WATU 63 wauawa katika shambulizi la kujitoa mhanga nchini Iraq

28 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCEv

Watu 63 wameuawa katika mjini wa Tal Afar, baada ya wanamgambo wa kujitoa mhanga kujilipua wakiwa na magari mawili kwenye soko moja.

Na wanamgambo wa Kisunni walijaribu kushambulia magari yaliyokuwa yakiwakimbiza hospitali mamia ya watu waliyojeruhiwa katika shambulizi hilo.

Shambulizi hilo linaashiria kurejea upya kwa uasi na machafuko katika mji huo unaokaliwa na washia wengi, mji ambao Rais George Bush aliuelezea kama ishara ya mafanikio ya majeshi ya Marekani mwaka mmoja uliyopita.

Katika hatua nyingine, Polisi wamesema kuwa kiasi cha watu 109 wameuawa kote Iraq katika siku mbili mbili zilizopita.

Wamesema kuwa katika tukio moja, gari lililipuka wakati watu walipokuwa wakinunua unga kaskazini magharibi mwa Baghdad ambapo watu 62 waliuawa na wengine zaidi ya 150 kujeruhiwa.

Wakati huo huo waandisi wawili na mwanajeshi mmoja wa Marekani wameuawa mjini Baghdad baada kufanyika shambulizi la roketi kwenye eneo lenye ulinzi mkali wa Marekani.

Taarifa ya ubalozi wa Marekani mjini Baghadad imesema kuwa watu wengine watano wamejeruhiwa wakiwemo waandisi wanne mmoja vibaya sana na askari mmoja.