Baghdad. Watu 28 wauwawa katika mlipuko wa bomu. | Habari za Ulimwengu | DW | 05.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Baghdad. Watu 28 wauwawa katika mlipuko wa bomu.

Kiasi watu 28 wameuwawa baada ya bomu lililokuwa katika gari kulipuka katika eneo lenye watu wengi katika mtaa wenye maduka ya vitabu mjini Baghdad.

Afisa wa usalama nchini Iraq amesema kuwa watu 66 wamejeruhiwa, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto.

Hapo mapema zaidi ya wanajeshi 1000 wa Iraq na wa Marekani walifanya msako wa nyumba kwa nyumba katika eneo ambalo ni ngome kuu ya wanamgambo wa Kishia mjini humo. Maafisa wa kijeshi wamesema kuwa wanajeshi hao hawakupata upinzani wowote wakati wakifanya msako huo katika kitongoji cha Sadr City, eneo ambalo linafanyiwa doria na wanamgambo wa Mehdi wakiongozwa na kiongozi wa kidini Moqtada al-Sadr.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com