BAGHDAD : Wasunni wajitowa katika serikali | Habari za Ulimwengu | DW | 01.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD : Wasunni wajitowa katika serikali

Mawaziri sita wa Kisuni na naibu Waziri Mkuu Salam al Zubaie wamejitowa kwenye serikali ya mseto ya Iraq leo hii kutokana na kutotimizwa kwa madai yao kadhaa.

Kujiuzulu kwao kunaiacha serikali ya Waziri Mkuu Nuri al Maliki na Washia na Wakurdi tu.Hatua hiyo ni pigo kwa serikali ya umoja wa kitaifa ya al Maliki na yumkini ikafanya mazungumzo kuwa magumu zaidi kati ya Washia na makundi ya Wasuni walio wachache.

Marekani imekuwa ikihimiza serikali ya Iraq kukubali sheria kadhaa zilizosanifiwa kushughulikia mashaka ya Wasunni na kupunguza umwagaji damu wa kikabila.

Habari zinasema miripuko mikubwa mitatu ya mabomu katika wilaya zenye watu wengi imeuwa watu 69 leo hii.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com