1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Washukiwa 60 wameuawa nchini Irak

9 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCuS

Jeshi la Marekani linasema vikosi vyake nchini Irak tangu siku ya Jumapili vimeua si chini ya watu 60 walioshukiwa kuwa wanamgambo.Hati iliyotolewa siku ya Jumatano imesema,wanajeshi wa Kimarekani wamewaua waasi 38 na kuwajeruhi 9 wengine katika mapambano yaliozuka siku ya Jumapili,kaskazini mwa mji mkuu Baghdad. Ikaongezea kuwa vikosi vya Marekani na vya Irak viliwaua wanamgambo wengine 8 baada ya kuvamiwa kwa ghafla siku ya Jumanne katika mji wa Dugmat ulio kama kilomita 45 kusini ya Kirkuk.Taarifa zingine zilizotolewa na Marekani zimesema,wengine 14 waliodhaniwa kuwa wanamgambo waliuliwa katika operesheni za siku ya Jumanne na Jumatano.