Baghdad. Wanajeshi watatu wa Marekani wauwawa. | Habari za Ulimwengu | DW | 15.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Baghdad. Wanajeshi watatu wa Marekani wauwawa.

Bomu lililotegwa kando ya barabara limelipuka na kuuwa wanajeshi watatu wa Marekani wakati wakifanya doria katika gari kusini mwa mji wa Baghdad nchini Iraq.

Wanajeshi hao watatu wameuwawa jana mchana wakati gari lao lilipokanyaga bomu hilo.

Mapema jeshi la Marekani lilitangaza kifo cha mwanajeshi mmoja ambaye alifariki jana baada ya kupata majeraha katika mapigano katika jimbo la Anbar magharibi ya Iraq.

Vifo hivyo vinafikisha idadi ya wanajeshi wa Marekani waliouwawa nchini Iraq tangu kuanza uvamizi March mwaka 2003 kufikia 2,759 kwa mujibu wa tarakimu zinazotolewa na wizara ya ulinzi ya nchi hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com