1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Wanajeshi wa Kiiraki wameuawa kwa makosa

9 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCku

Nchini Irak,bomu lililotegwa ndani ya gari, limeripuka Kerbala,mji mmojawapo ulio takatifu kwa Washia.Si chini ya watu 8 wamefariki na 30 wengine wamejeruhiwa.Wakati huo huo,wakazi wa Doluiya,kama kilomita 80 kaskazini ya mji mkuu Baghdad wamesema,wanajeshi wa Kimarekani kwa makosa waliwaua wanajeshi 3 wa Kiiraki katika operesheni ya uvamizi iliyofanywa katika eneo hilo.