1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Wanadiplomasia waliokamatwa nchini Iraq watembelewa.

8 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBkx

Wanadiplomasia wa Iran wamefanya ziara ya kwanza ya kibalozi kuwaona Wairan watano wanaoshikiliwa na majeshi ya Marekani nchini Iraq tangu walipokamatwa Januari mwaka huu.

Jeshi la Marekani limesema watu hao watano wanahusishwa na jeshi la kimapinduzi la Iran na walikuwa wanawaunga mkono wapiganaji nchini Iraq.

Iran imekuwa ikisisitiza kuwa watu hao walikuwa ni wanadiplomasia wake, na kudai waachiwe huru na kuomba kupata kuonana nao.

Marekani inaishutumu Iran kwa kuwapatia silaha , fedha na mafunzo ya kijeshi wapiganaji wa Kishia nchini Iraq.