1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Wairaq waambiwa kuwa hawatasaidiwa daima na Marekani.

21 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC8a

Katika siku yake ya pili ya ziara yake ya ghafla nchini Iraq, waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates amekuwa na mazungumzo na viongozi wa Iraq, ikiwa ni pamoja na waziri mkuu Nouri al – Maliki.

Gates amewaambia kuwa juhudi zinapaswa kuongezwa kuondoa tofauti baina ya makundi hasimu ya kidini ya nchi hiyo.

Marekani inaongeza mbinyo kwa serikali inayoongozwa na Washia ya Maliki kuingia katika makubaliano ya kugawana madaraka na Wasunni katika juhudi za kupunguza ghasia.

Gates pia amesema kuwa juhudi za Marekani nchini Iraq zina ukomo.

Ziara yake ni ya kwanza tangu mpango unaungwa mkono na Marekani wa usalama kwa ajili ya mji wa baghdad kuanzishwa mwezi wa Februari ukihusisha wanajeshi 20,000 wa ziada.