1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Wafuasi wa al Sadr wajiondoa serikalini

16 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPW

Wabunge 30 walio watiifu kwa Muqtada al Sadr wametangaza wanajiondoa kutoka kwa muungano wa Kishia katika bunge la Irak wakipinga kukamatwa kwa wafuasi wa shehe huyo wanaoipinga Marekani.

Uamuzi huo unaidhoofisha serikali ya waziri mkuu Nuri al Maliki ambayo imeshindwa kupitisha sheria zinazolenga kuwapatanisha warabu wa madhehebu ya Shia na Sunni nchini Irak.

Kuondoka kwa wafuasi wa Moqtada al Sadr kutoka kwa muungano wa Washia huenda ukazikwamisha juhudi zinazoungwa mkono na Marekani za kutaka mswada wa sheria wa kugawana madaraka upitishwe na bunge. Mswada huo unahusu kugawana pia faida inayotokana na utajiri wa mafuta na kulegeza sheria zinazowazuia wafuasi wa rais wa zamani wa Irak, Saddam Hussein, wasipate kazi zao serikalini.

Wakati haya yakiarifiwa mshambuliaji wa kujitoa mhanga maisha amejilipua na kuwaua watu 10 katika kitongoji cha Amil mjini Baghdad. Watu wengine 15 wamejeruhiwa katika hujuma hiyo.