BAGHDAD: Wabunge wafuasi wa Moqtada al-Sadr kurejea bungeni
21 Januari 2007Matangazo
Kundi la wabunge wafuasi wa kiongozi wa Kishia Moqtada al-Sadr nchini Iraq limekubali kurejea bungeni baada ya kulisusia bunge hilo kwa muda wa miezi miwili.
Kundi hilo ni mshirika muhimu wa Waziri Mkuu wa Iraq, Nouri al-Maliki, lakini limekuwa likisusia vikao vya bunge tangu mwezi Novemba mwaka uliopita likitaka majeshi ya Marekani kuondoka nchini humo.
Kundi hilo pia lilisusia bunge kupinga mkutano uliofanyika kati ya Nouri al-Maliki na Rais wa Marekani, George W. Bush..
Marekani inalichukulia kundi la wanamgambo la Mahdi linaloongozwa na Moqtada al-Sadir kuwa tishio kubwa la usalama nchini Iraq.