1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Waandishi wa habari 2 wameuawa nchini Irak

4 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMP

Mamia ya wanajeshi wa Kimarekani wameingia Sadr City,eneo linalojulikana kama ni ngome ya Washia katika mji wa Baghdad.Maafisa wa Kimarekani wamesema,vikosi havijakabiliana na upinzani vilipokuwa vikisaka nyumba moja moja katika mtaa huo,ambao hudhibitiwa na wanamgambo wa “Jeshi la Mahdi“ linaloongozwa na shehe mwenye msimamo mkali,Moqtada al-Sadr.Na ripoti za hivi punde zinasema,wanamgambo nchini Irak wamewaua waandishi wa habari wawili.Mhariri mkuu wa gazeti huru „Al Mashrek“ alipigwa risasi mbele ya nyumba yake mjini Baghdad.Hapo awali,maiti ya mwandishi wa habari wa gazeti la „Al Safir“ ilipatikana Baghdad.Yeye alitoweka siku chache za nyuma.