1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Umwagaji wa damu unaendelea nchini Irak

5 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbp

Wimbi la machafuko linaendelea nchini Irak.Mapema leo hii,mizinga ilivurumishwa kwa mfululizo katika kituo cha petroli kilichokuwa kimejaa watu.Mashambulizi hayo yameua watu 11 na kujeruhi wengine 15.Magari mengi pia yaliteketezwa.Mizinga mingine pia ilianguka kwenye kituo kingine cha petroli karibu na hapo na kuwajeruhi watu sita.

Wakati huo huo,vikosi vya Marekani na vya serikali ya Irak,vimedai kuwa hii leo vilifanikiwa kawashinda wanamgambo wa Al-Qaeda. Maafisa wa kijeshi wamesema,vikosi vya Irak viliwakamata washukiwa ugaidi 80 wakati wa operesheni ya usalama,iliyoanza tarehe 31 mwezi Julai.