1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Takriban watu 47 wameuwawa katika shambulio la bomu

14 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9y

Mpiganaji wa kujitoa muhanga amejilipua katika mji mtakatifu wa Karbala karibu na maeneo ya madhabahu ya Kishia kilomita 80 kusini mwa mji wa Baghdad.

Takriban watu 47 wameuwawa katika shambulio hilo, kwa mujibu wa taarifa za polisi na duru za hospitali watu wengine 70 wamejeruhiwa wengi wao ni wanawake na watoto.

Shambulio hilo limetokea hatua chache tu karibu na madhabahu ya Imam Hussein mahala alipozikwa mjukuu wa mtume Muhammad S.A.W.

Karbala ni mji mtukufu kwa waumini wa madhehebu ya Kishia ambao humiminika kufanya hija katika mji huu kila mwezi wa tatu.

Waandamanaji wamezingira ofisi ya gavana wa jimbo hilo wakidai ajiuzulu kutokana na kuzembea katika maswala ya usalama.

Wakati huo huo Marekani imesema kwamba ina imani kuwa vikosi vya usalama vya Irak vina uwezo wa kulinda nyenzo za serikali licha ya shambulio la bomu la alhamisi katika eneo la bunge la Irak.