BAGHDAD: Shambulizi la kujitolea muhanga lasababisha hadi vifo 30 | Habari za Ulimwengu | DW | 07.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Shambulizi la kujitolea muhanga lasababisha hadi vifo 30

Watu wasiopungua 30 wameuawa katika mripuko wa bomu lililotegwa ndani ya gari,katika eneo la sokoni mjini Tuz Khurmato,kaskazini mwa Iraq.Kwa mujibu wa polisi,watu 80 vile vile walijeruhiwa katika shambulizi hilo la kujitolea muhanga kwenye soko la hadhara lililojaa watu.Mripuko huo pia umeteketeza idadi kadhaa ya majengo yaliokuwepo karibu na eneo hilo.Inahofiwa kuwa huenda ikawa watu wamegubikwa na vifusi vya majengo yaliyoporomoka.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com