BAGHDAD: Shambulio lingine la kujitolea muhanga nchini Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 19.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Shambulio lingine la kujitolea muhanga nchini Irak

Hadi watu 17 wameuawa katika shambulio la bomu la kujitolea muhanga lililotokea katika mji wa Hilla nchini Irak.Zaidi ya watu 40 pia walijeruhiwa katika shambulio hilo lililofanywa kama kilomita 120 kusini mwa mji mkuu Baghdad.Kwa mujibu wa polisi,mshambulizi aliekuwa ndani ya gari aliripua bomu kati kati ya kundi la watu waliokuwa wakifanyakazi za ujenzi.Katika shambulio jingine,mwanasiasa mashuhuri wa Kishia Ali al-Adhadh wa Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiislamu,aliuawa pamoja na mkewe kwa kupigwa risasi,walipokuwa wakipita kwa gari mjini Baghdad.Shambulio hilo lilitokea wakati ambapo vikosi vya Kimarekani na vya madola shirika vilikuwa vikiwasaka watu waliotekwa nyara kusini mwa Irak na katika mtaa wa Sadr City ukingoni mwa mji mkuu Baghdad.Msako huo ulianzishwa baada ya vikosi hivyo kugundua maiti ya Mmarekani alietekwa nyara na kuweza kuwakomboa wengine wawili katika uvamizi uliofanywa siku ya Ijumaa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com