BAGHDAD : Sadr hakukimbilia Iran | Habari za Ulimwengu | DW | 15.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD : Sadr hakukimbilia Iran

Sheikh wa msimamo mkali wa Kishia Moqtada al Sadr yuko katika ziara fupi nchini Iran.

Afisa wa serikali ya Iraq amekanusha kwamba sheikh huyo anayepinga Marekani amekimbia msako wa Marekani nchini Iraq kama ule unaohusu Jeshi lake la Mehdi lenye kuhofiwa nchini humo.

Sami al Askari msaidizi wa waziri mkuu wa Iraq Nuri al Maliki akithibitisha madai yaliobishiwa ya jeshi la Marekani ameshutumu Wamarekani kwa kuchochea utata juu ya suala hilo.

Msemaji wa jeshi la Marekani nchini Iraq Meja Generali William Caldwell alizungumzia suala hilo na mapema.

Wafuasi wa Al Sadr walikanusha tangazo la jeshi la Marekani kwamba kiongozi wao huyo alikuwa ameondoka kueleka Iran mwezi uliopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com