1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Saddam Hussein arudishwa mahakamani katika kesi ya pili ya kuwaangamiza wakurudi

7 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCv5

Rais wa zamani wa Irak, Saddam Hussein, amerudishwa mahakamani mjini Baghadad ikiwa ni siku mbili tu baada ya kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa hatia ya uvunjaji haki za binaadamu. Kiongozi huyo wa zamani wa Irak na washirika wake 6, safari hii wanatuhumiwa kwa mauaji ya kuangamiza wakurdi katika kijiji cha Anfal katika kile kilichotajwa ´´Anfal campaign´´ ambapo takriban watu 180,000 waliuawa. Saddam Hussein, alikata rufaa dhidi ya hukumu ya kifo iliotolewa katika kesi ya kwanza kuhusu mauaji ya washiha 148 mwaka wa 1982 na haijajulikana ikiwa hukumu hiyo itathibitishwa na mahakama ya rufaa, itaweza kutekelezwa kabla ya kukatwa kesi hiyo ya pili juu ya mauaji ya wakurdi.