BAGHDAD: Rice amefanya ziara ya ghafula Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 17.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Rice amefanya ziara ya ghafula Irak

Waziri wa masuala ya nje wa Marekani,Condoleezza Rice akiwa njiani kuelekea Israel,ametua katika mji mkuu wa Irak,Baghdad.Rice ametaka kukutana na waziri mkuu wa Irak Nouri al-Maliki na pia wajumbe wa Kimarekani na Kiiraki.Baadae leo hii nchini Israel,atakutana na waziri mwenzake Tzipi Livni.Hiyo kesho atakuwa na mikutano miwili mbali mbali pamoja na Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert na rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas kwa matayarisho ya mkutano wa kilele wa pande tatu uliopangwa kufanywa siku ya Jumatatu.Katika mkutano huo,Rice atashauriana na viongozi hao juu ya misingi ya taifa la Palestina la siku zijazo. Serikali mpya ya Wapalestina ya umoja wa kitaifa vile vile ni miongoni mwa mada zitakazojadiliwa. Waziri mkuu mteule wa Wapalestina,Ismail Haniyeh amesema,katika muda wa hadi majuma matatu yajayo, anatazamia kuwa tayari na serikali hiyo mpya.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com