1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Rais wa zamani wa Irak, Saddam Hussein awaita raia kuyafukuza majeshi ya kigeni

17 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD29

Rais wa zamani wa Irak, Saddam Hussein, amewatolea mwito raia wa Irak waache kando tofauti zao na waungane kuwafukuza wanajeshi wa kigeni kutoka nchi yao. Mwito huo umetolewa katika barua Saddam Hussein aliyoiandika gerezani. Alisema raia wa Irak wasipotoshwe na mauaji yanayoendelea na badala yake yawafukuze wanajeshi wa kigeni. Mauaji hao yanaendelea.

Mdogo wake mwendeshamshitaka mkuu katika kesi ya mauaji ya kuangamiza jamii inaomkabili rais wa zamani, Saddam Hussein, amepigwa risasi na kuuawa. Imad al- Faroon, aliuawa na watu waliokuwa na bunduki nje ya nyumba yake magharibi mwa mji mkuu Baghdad. Kwa jumla jana watu 30 waliuawa katika mlolongo wa miripuko ya mabomu yaliyotegwa ndani ya gari. Shambulio baya zaidi lilitokea katika sehemu kunakoishi watu wa mchanganyiko wa kidini kaskazini mwa mji mkuu Baghdad na kuwauwa watu 20. Tangu mwezi Februari mwaka huu, machafuko kati ya Wasuni na Washiha yameshasababisha mauaji ya maelfu ya watu na wengine kiasi ya 300,000 waliolazimika kuyahama maskani yao. Marekani kwa upande wake, imewapoteza wanajeshi wengine watatu na hivyo kufikisha idadi ya wanajeshi wake waliouawa nchini Irak mwezi huu pekee yake, kuwa 56.