1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Raia na wanamgambo wauawa na vikosi vya Marekani

3 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCn2

Vikosi vya Marekani nchini Irak,vimewaua wanawake wawili,mtoto mmoja na watu sita walioshukiwa kuwa wanamgambo katika operesheni ya angani,magharibi mwa mji mkuu Baghdad.Jeshi la Kimarekani limeripoti leo hii kuwa uvamizi huo uliofanywa Jumamosi usiku,ulilenga mji wa Gharma ulio kati ya Baghdad na Fallujah unaosemekana kuwa ni ficho la wanamgambo.Raia waliouawa sasa ni wahanga wapya,baada ya wasichana watano kuuawa juma hili kwa risasi zilizofyatuliwa na vifaru kuwalenga wanamgambo mjini Ramada na pia wanawake wawili kuuawa kaskazini mwa Baghdad katika shambulio jingine la angani lililofanywa dhidi ya wanamgambo.