1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Raia 42 waachiwa huru.

28 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxX

Majeshi ya Marekani yamewaacha huru Wairaqi 42 waliokuwa wamekamatwa na kundi la al-Qaeda kaskazini ya mji wa Baghdad.

Jeshi la Marekani limesema kuwa baadhi ya watu hao wameshikiliwa na kuteswa kwa muda wa miezi kadha.

Msemaji wa jeshi hilo amesema kuwa operesheni imezinduliwa katika jimbo lenye matatizo la Diyala baada ya wakaazi wa eneo hilo kutoa taarifa.

Pia katika jimbo hilo la Diyala , bomu lililotegwa kando ya barabara limesababisha kifo cha mwanajeshi mmoja wa Marekani na mwanajeshi wa pili ameuwawa katika mlipuko uliotokea mjini Baghdad.