1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad: Mwanajeshi wa Kiengereza auwawa mjini Baghdad, Iraq

28 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCNk

Mwanajeshi wa Kiengereza ameuwawa alipokuwa akipiga doria kusini mwa Iraq. Wizara ya ulinzi ya Uengereza ilisema mwanajeshi huyo aliuwawa wakati yalipofanywa mashambulio madogo ya bunduki huko Basra. Wiki iliopita, waziri mkuu wa Uengereza, Tony Blair, alisema idadi ya wanajeshi wa Kiengereza huko Iraq itapunguzwa mnamo miezi michache ijayo. Mwanzoni leo, mripuko wa bomu lilotegwa ndani ya gari lilitikisa soko kubwa mjini Baghdad na kuwauwa watu 10 na kuwajeruhi wengine saba. Polisi wa Iraq wanasema bomu hilo liliripuka katika mtaa wa Bayaa, kusini mwa Baghdad.

Kwa upande mwengine, wanajeshi wa Kimarekani wamewauwa watu wanane wanaoshukiwa kuwa ni wapiganaji wa kigaidi na kuwakamata sita wengine katika msako waliofanya katika mji mkuu wa Iraq. Jeshi la Marekani lilisema msako huo umelengewa mtandao wa al-Qaida huko Iraq pamoja na wenyeji wanaoshukiwa wanawahifadhi wapiganaji wa kigaidi.