1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Mripuko mkubwa umeua watu 75 nchini Iraq

19 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqC

Shambulio la kujitolea muhanga karibu na msikiti wa madhehebu ya Kishsia katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad umeua si chini ya watu 75 na wengi wengine wamejeruhiwa.Sehemu kubwa ya msikiti pia imeteketezwa.Kwa mujibu wa polisi,mripuko wa mabomu yaliotegwa ndani ya lori,ulitikisa sehemu za kati kati za mji mkuu Baghdad.Shambulio hilo limetokea siku mbili baada ya kuondoshwa amri ya kuwazuia watu kutoka majumbani mwao.Amri hiyo ilitangazwa kufuatia shambulio lililofanywa juma lililopita,dhidi ya msikiti muhimu wa waumini wa Kishia katika mji wa Samarra.