1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Mmuagiko wa damu unaendelea Irak

22 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0E

Idadi kubwa ya watu wameuawa nchini Irak katika shambulio lililofanywa sokoni mjini Mahmudiya. Kituo cha televisheni cha Kiarabu “Al Jazeera” kimeripoti si chini ya vifo 30.Wizara ya ulinzi ya Irak imesema ni watu 20 waliouawa katika shambulio hilo ambapo mshambuliaji asiejulikana alifunga mabomu kwenye idadi kadhaa ya baiskeli. Na mjini Baghdad shambulio la kujitolea muhanga kwenye basi limeua watu wanne. Wanajeshi watatu wa Kimarekani pia waliuawa katika mapambano yaliotokea na waasi kwenye wilaya ya Anbar.