1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Mauaji yameongezeka maradufu mjini Baghdad.

26 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVv

Ongezeko la majeshi ya Marekani nchini Iraq linasemekana kuwa limepunguza ghasia mjini Baghdad kutoka kiwango cha juu , lakini idadi ya watu wanaouwawa kutokana na mashambulizi ya kimadhehebu nchi nzima inaongezeka mara dufu ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Baadhi ya mauaji ya hivi karibuni yanaonekana kuwa ni matokeo ya wapiganaji kukimbilia katika maeneo ya kaskazini ya Iraq, ambako wanakimbilia baada ya majeshi ya Marekani kuongeza mashambulizi yao.

Mjini Baghdad hata hivyo , inapata zaidi ya nusu ya vifo vinavyosababishwa na vita , ikiwa ni asilimia ile ile kama mwaka uliopita, kwa mujibu wa takwimu zilizopatikana na shirika la habari la Associated Press.

Kwa mujibu wa wadadisi wa masuala ya kisiasa nchini Iraq upande wa majeshi ya Uingereza nchini humo umefanyakazi nzuri kuliko ule wa majeshi ya Marekani.

Hali imekuwa taratibu ikizidi kuharibika baada ya kutokea kile kinachoonekana kama vita vya makundi ya kihalifu pamoja na ukosefu wa udhibiti wa polisi katika aina hiyo ya ghasia. Hali inaendelea kuwa mbaya.

Baada ya majeshi ya Marekani kuongezwa wanajeshi 30,000 yalianza kampeni yao mwezi Februari kuchukua udhibiti wa eneo la mji wa Baghdad .