1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Mashambulio yaendelea kupoteza maisha

8 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLH

Si chini ya watu 55 wameuawa katika mashambulio mbali mbali nchini Irak.Watu 30 walipoteza maisha yao katika mji wa Balad Ruz baada ya mshambulizi aliejitolea muhanga kujiripua ndani ya mkahawa mmoja.Na katika mji mkuu Baghdad,zaidi ya watu 20 waliuawa katika mripuko wa bomu.Shambulio hilo limetokea siku moja baada ya mahujaji 120 wa madhehebu ya Kishia kuuawa mjini Hillah katika mashambulio mawili ya kujitolea muhanga.Waumini hao walishambuliwa walipokuwa njiani kwenda mji takatifu wa Kerbala kushiriki katika sherehe za kidini.