Baghdad. Majeshi ya Marekani yauwa watu watano. | Habari za Ulimwengu | DW | 08.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Baghdad. Majeshi ya Marekani yauwa watu watano.

Majeshi ya Marekani yamewauwa watu watano wanaoshukiwa kuwa ni wapiganaji na kuwakamata wengine watatu katika eneo wanaloishi Washia katika kitongoji cha mjini Baghdad cha Sadr City. Taarifa ya jeshi la Marekani imesema kuwa lengo la shambulio hilo ni kamanda wa makundi maalum, anayeshukiwa kuwa anahusika na kuwakamata watu pamoja na mashambulio ya mabomu katika mji mkuu wa Iraq. Jeshi hilo limesema makundi hayo maalum , jina linalotumika kwa maana ya makundi ya siri ya Washia, yanauhusiano wa karibu na wanamgambo wa jeshi la Mahdi la kiongozi wa kidini mwenye msimamo mkali Moqtada al-Sadr.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com