1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Mabomu yalipuka kwa pamoja na kuuwa watu kadha.

5 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmQ

Mabomu matatu katika magari yaliyolipuka wakati mmoja karibu na kituo cha kuuzia mafuta kusini mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad, na kuuwa kiasi watu 14 na kuwajeruhi wengine 25.
Shambulio hilo lilifanyika katika kitongoji cha Washia cha Bayaa.
Katika tukio tofauti, wafanyakazi 15 wa kidini wa Kishia wameuwawa katika shambulio la ghafla katika basi walilokuwa wakisafiria kaskazini ya mji huo.
Maafisa wa usalama wamesema watu wenye silaha kwanza walifyatua bomu katika gari kabla ya kufyatua risasi dhidi ya basi hilo.
Wakati huo huo jeshi la Marekani limesema kuwa wapiganaji wameshambulia kituo cha doria cha jeshi la Marekani mjini Baghdad, na kumuua mwanajeshi mmoja na kumjeruhi mwingine. Taarifa hiyo imesema mwanajeshi mwingine pia ameuwawa jana Jumatatu akiwa katika gari.