1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Maafa yaendelea kutokea Iraq

2 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvd

Duru za kiusalama za Iraq zimesema bomu lililotegwa ndani ya lori limelipuka na kuwaua askari kumi na mmoja wa nchi hiyo katika mji wa kaskazini wa al-Sharkat.

Majeshi ya Marekani yamesema watoto watatu waliuawa kwenye shambulio dhidi ya wanamgambo katika jimbo la Anbar.

Majeshi hayo yaliwafyatulia risasi watu watatu wanaosemekana walikuwa wakitega mabomu kwenye barabara moja kuu kusini mashariki mwa Fallujah, kiasi kilomita sitini na tano magharibi mwa Baghdad.

Haijajulikana moja kwa moja ikiwa watoto hao walifariki kutokana na shambulio hilo au milipuko iliyofuatia baadaye lakini majeshi hayo yamesema uchunguzi ungali ukiendelea.

Kwengineko, askari wa Marekani ameuawa kwa kupigwa risasi katika eno la kati la Baghdad.

Mjini Baquba, mtu aliyejitoa mhanga alijilipua katika jumba linalowahifadhi wanamgambo walioamua kuachana na vita.

Watu wawili walifariki kwenye tukio hilo.