1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Kundi la Al Qaeda ladai kuwaua wanajeshi wa Marekani

24 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7W

Kundi la Al- qaeda nchini Irak limedai kuhusika na shambulio lililowaua wanajeshi tisa wa Marekani.

hapo awali jeshi la Marekani nchini Irak lilitangaza kwamba wanajeshi wake tisa wameuwawa na wengine 20 kujeruhiwa kwenye shambulio la bomu lililofanywa na mtu wa kujitoa mhanga maisha kaskazini mashariki mwa mji mkuu Baghdad.

Hujuma hiyo ilitokea katika mkoa wa Diyala ambako wanajeshi wa Marekani wamekuwa wakikabiliwa na mashambulio makali ya wapiganaji wa Irak.