1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Kouchner ziarani Irak

20 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXN

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ufaransa, Bernard Kouchner, leo amekutana na rais wa Irak, Jalal Talabani, kiongozi wa Wakurdi, Massoud Barzani na maafisa wengine wa Irak.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Baghdad, Bernard Kouchner, amesema Umoja wa Mataifa huenda ukawa na jukumu kubwa katika kutafuta ufumbuzi wa kisiasa miongoni mwa makundi yanayohasimiana nchini Irak.

Bwana Kouchner ni waziri mkuu wa kwanza wa Ufaransa kuitembelea Irak tangu uvamizi wa Irak ulioongozwa na Marekani ambao ulipingwa vikali na serikali ya Ufaransa.

Alipowasili mjini Baghdad hapo jana waziri Kouchner aliahidi kwamba Ufaransa itaisidia Irak kumaliza machafuko yanayoendelea nchini humo, hatua inayoashiria juhudi mpya za kuboresha uhusiano kati ya Ufaransa na Marekani.