BAGHDAD: Kiongozi mashuhuri wa Kisunni ameuawa Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 13.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Kiongozi mashuhuri wa Kisunni ameuawa Irak

Kiongozi mashuhuri wa madhehebu ya Kisunni Abdel-Sattar Abu Risha ameuawa katika shambulizi la bomu nchini Irak.Kwa mujibu wa stesheni ya televisheni ya al-Iraqiya,bomu lililotegwa karibu na nyumba yake mjini Ramadi katika wilaya ya Anbar,limemuuwa Abu Risha pamoja na walinzi wawili na karani wake.

Juma lililopita,Rais wa Marekani George W.Bush alipokwenda Irak,alikutana na Abu Risha na alimshukuru kwa ushirikiano wake kuwapiga vita wanamgambo wa Al-Qaeda.Abu-Risha aliunganisha makundi ya makabila mbali mbali katika wilaya ya Anbar kwa azma ya kupambana na Al-Qaeda nchini Irak.Wadadisi wanaamini kuwa baada ya Wamarekani, Abu Risha alieongoza Baraza la Uokozi wa Anbar, alitazamwa na Al-Qaeda kama ni adui wao wa pili.Hali ya hatari imetangazwa katika mji wa Ramadi ulio umbali wa kilomita 110 kutoka mji mkuu Baghdad.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com