BAGHDAD : Gates afanya ziara ya ghafla Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 20.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD : Gates afanya ziara ya ghafla Iraq

Waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates amewaambia viongozi wa Iraq kwamba lazima waimarishe juhudi zao za kufanikisha usuluhishi kati ya makundi ya kimadehebu.

Gates ametowa kauli hiyo mjini Baghad baada ya kuwasili katika mji mkuu huo wa Iraq na mapema katika ziara ambayo haikutangazwa.Hii ni ziara ya tatu ya Gates nchini Iraq na ya kwanza tokea Rais George W. Bush kutuma vikosi vya ziada 20,000 huko Baghdad katika juhudi za kukomesha umwagaji damu mjini humo.

Ziara yake inakuja siku moja baada ya miripuko kadhaa ya mabomu kuuwa takriban watu 200 wakiwemo 140 katika soko la chakula.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com