1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Brown azuru majeshi .

3 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKf

Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown amesema kuwa kiasi cha wanajeshi 1,000 kati ya wanajeshi 5,000 wa nchi hiyo ambao wako nchini Iraq huenda wakaondolewa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Brown alikuwa akizungumza wakati wa ziara yake ya kwanza nchini Iraq tangu kushika wadhifa wa waziri mkuu mapema mwaka huu. Brown amekutana na waziri mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki mjini Baghdad. Amewaambia waandishi wa habari kuwa majeshi ya Iraq yatakuwa tayari kuchukua jukumu la usalama kutoka majeshi ya Uingereza katika jimbo la Basra katika muda wa miezi miwili ijayo. Brown alikuwa anatarajiwa kukutana na makamanda wa kijeshi wa jeshi la Marekani nchini Iraq.