BAGHDAD: Blair afanya ziara ya ghafula Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 19.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Blair afanya ziara ya ghafula Iraq

Tony Blair anaeondoka madarakani mwezi Juni, anafanya ziara yake ya saba na ya mwisho nchini Iraq,kama waziri mkuu wa Uingereza.Wakati wa ziara hiyo,Blair anatarajiwa kutoa wito wa kufanywa chaguzi mpya za majimbo na kuimarisha juhudi za kuwaingiza katika mfumo wa kisiasa,wale wanaohusika na machafuko nchini Iraq.Blair aliefanya ziara hiyo bila ya kutangazwa hapo awali,vile vile anatazamiwa kumhakikishia Waziri Mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki kuwa kuondoka kwake madarakani mwezi ujao,hakutomaanisha kuwa ni mwisho wa msaada wa Uingereza.Blair,ambae uongozi wake uliandamwa na uamuzi wa utata wa kujiunga na uvamizi wa Iraq mwaka 2003 kumuondosha madarakani Saddam Hussein,aliwasili Iraq kupitia Kuwait. Siku ya Alkhamisi Blair alikuwepo Washington kwa majadiliano pamoja na Rais George W.Bush wa Marekani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com