1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD :Baadhi ya mahabusu wameachiliwa huru

15 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsf

Watu darzeni kadhaa wameachiliwa huru kutoka lile kundi la watu lililotekwa nyara katika taasisi ya utafiti mjini Baghdad.Ripoti za vyombo vya habari vilivyonukulu wizara ya mambo ya ndani ya Irak zimesema,mahabusu wengi ama waliachiliwa huru au waliokolewa na vikosi vya serikali sehemu mbali mbali za Baghdad.Bado haijulikani hasa ni watu wangapi waliotekwa nyara.Baadhi ya maafisa wanasema ni zaidi ya watu 100,huku wengine wakisema kama watu 60 walichukuliwa mahabusu. Utekaji nyara huo ulifanywa mchana kweupe na watu wenye silaha waliovaa sare za polisi.Maafisa wa polisi 5 wa ngazi ya juu wamekamatwa,huku polisi wakilaumiwa kwa jinsi walivyoshughulikia hali ya usalama katika eneo la utekaji nyara huo.Waziri wa elimu ya juu wa Irak,Abed Dhiyab al-Ajili ametoa amri ya kuvifunga vyuo vikuu vyote mpaka hali ya usalama itakapokuwa nzuri.Wakati huo huo, zaidi ya watu 100 waliuawa nchini Irak katika mashambulio na mapigano mapya yaliozuka siku ya Jumanne.