BAGHDAD: Askari zaidi wa Marekani wauawa nchini Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 31.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Askari zaidi wa Marekani wauawa nchini Iraq

Askari watatu wa Marekani wameuawa nchini Iraq hapo jana, katika mapambano na wanamgambo wa Kisunni.

Mapambano hayo yalitokea kwenye jimbo la Anbar lililoko magharibi mwa Iraq, ambako ni moja kati ya maeneo yaliyokumbwa na vurugu za wanamgambo hao.

Kati ya askari wa ziada elfu 21 wa Marekani watakaopelekwa Iraq, elfu 4 watapelekwa katika jimbo hilo.

Kuawa kwa askari hao kumefanya askari wa Marekani waliyokufa mpaka sasa toka nchi hiyo ilipoivamia Iraq Marcha mwaka 2003 kufikia elfu 3 na 78.Hii ni kwa mujibu wa takwimu za wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon.

Wakati huo huo mkuu mpya mtarajiwa wa majeshi ya Marekani katika mashariki ya kati, Admiral William Fallon ametaka kuwepo kwa mtizamo mpya katika Iraq.

Admiral Fallon alikimbia kikao cha Maseneta huko Marekani kwamba, nchi hiyo inakimbiwa na muda kuweza kurejesha hali ya mambo nchini Iraq.

Aidha aliilaumu Iran kuwa imekuwa ikichangia kuharibika kwa amani katika eneo la mashariki ya kati.

Katika hatua nyingine mauaji yameendelea kutokea nchini Iraq ambapo zaidi watu hamsini wameuawa wakati wa siku ya mwisho ya kumbukumbu ya Ashura ambayo ni siku takatifu kwa waumini wa madhehebu ya shia.

Kiasi cha watu 23 waliauawa na wengine zaidi ya sitini kujeruhiwa wakati mlipuaji wa kujitoa mhanga aliposhambulia msikiti wa washia huko Mandali.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com