1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Al- Maliki ataka mkutano wa kisiasa

13 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZr

Waziri Mkuu wa Iraq Nuri al Maliki ametowa wito wa kufanyika kwa mkutano wa kilele wa viongozi wa kisiasa nchini humo.

Al- Maliki ambaye serikali yake imedhoofishwa kutokana na mapigano ya ndani ya nchi amesema anataraji viongozi wa kisiasa kujadili mchakato wa kisiasa katika mkutano utakaofanyika katika siku chache zijazo.Wakati huo huo kiongozi wa Kisunni ametowa wito wa msaada kwa nchi za Kiarabu dhidi ya kile alichokiita uungaji mkono wa Iran kwa vikosi vya mauaji na wanamgambo.Adnan al- Dulaimi kiongozi wa kundi kubwa la Masunni katika bunge ameonya kwamba Baghdad iko hatarini kuangukia kwenye mikono ya Waajemi na Masafawis akimaanisha Iran.

Takriban nchi zote majirani wa Iraq wana idadi kubwa ya Waislamu wa madhehebu ya Sunni wakati Iran na Iraq wana idadi kubwa ya Waislamu wa madhehebu ya Shia jambo ambalo linazusha wasi wasi juu ya ushawishi wa serikali ya Iran juu ya serikali ya Iraq na vikosi vyake vya usalama inavyohodhiwa na Washia.