1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Auwa wanane kabla ya kujiuwa mwenyewe

6 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CYOH

OMAHA –Marekani

Kijana alietaka kufa akiwa mtu maarufu amewauwa kwa kuwapiga risasi watu wanane na kujeruhi wengine katika jengo la maduka mengi la Omaha kabla ya kujiuwa mwenyewe.

Robert Hawkins mwenye umri wa miaka 19 aliacha baruwa yenye maelezo ya kujiuwa kwake.

Wafanyakazi walikimbia kwa kiwewe kutoka jumba hilo la maduka mengi la Westroads au kujifungia ndani ya maduka baada ya kusikia risasi zikidata ovyo.